Psalms 4

Sala Ya Jioni Ya Kuomba Msaada

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi.

1 aNijibu nikuitapo,
Ee Mungu wangu mwenye haki!
Nipumzishe katika shida zangu;
nirehemu, usikie ombi langu.

2 bEnyi watu, mtabadilisha utukufu wangu
kuwa aibu mpaka lini?
Mtapenda udanganyifu
na kufuata miungu ya uongo mpaka lini?
3 cFahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga
wale wamchao kwa ajili yake;
Bwana atanisikia nimwitapo.

4 d eKatika hasira yako, usitende dhambi.
Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya
mkiichunguza mioyo yenu.
5 f gToeni dhabihu zilizo haki;
mtegemeeni Bwana.

6 hWengi wanauliza, “Ni nani awezaye
kutuonyesha jema lolote?”
Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.
7 iWewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa
kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.
8 j kNitajilaza chini na kulala kwa amani,
kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana,
waniwezesha kukaa kwa salama.
Copyright information for SwhNEN